• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Sunday, May 7, 2017

    BASI LILILOUA WANAFUNZI LILING'OKA VITI VYOTE.

    Image result for mteremko mkali

    Inasemekana kuwa basi dogo lilopata ajali na kusababisha vifo zaidi ya 35 lilikuwa limeng'oka viti vyote mara baada ya ajali hiyo.Akizungumza na TBC 1 muda mfupi uliopita katika kipindi maalumu kilichoandaliwa na TBC 1,kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa arusha kamanda suleimani amesema basi hilo liling'oka viti vyote ishara kwamba lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi.
     Pia inasadikika kuwa basi hilo dogo lilikuwa ni jipya na dereva wake pia alikuwa ni mgeni katika njia hiyo.Hata hivyo kamanda sulemani amesema eneo ambalo ajali hiyo imetokea kuna alama zote zinazoonyesha hali ya barabara ikiwemo ile inayoonyesha mteremko mkali.Pia kamanda suleimani amesema basi hilo lilikuwa na mikanda ya usalama japo ni vigumu kujua kama ilikuwa imefungwa na wanafunzi hao.
       kwa upande mwingine makamu wa raisi samia suluhu hassan  atawaongoza watanzania kuaga miili ya marehemu hapo kesho katika uwanja wa sheik amri abeid jijini arusha.
    Kibayaclassic inaendelea kuungana na watnzania wote katika kipindi hiki kigumu.

    No comments:

    Post a Comment