• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Friday, May 5, 2017

    Abbas Abdullahi Siraji amezikwa katika mazishi ya kitaifa.

    Image result for Abbas Abdullahi Siraj
    Waziri wa ujenzi nchini Somalia aliyeuawa  na mwanajeshi wa serikali mjini Mogadishu siku ya Jumatano Abbas Abdullahi Siraji amezikwa katika mazishi ya kitaifa.
    Mmoja wa wanajeshi wa serikali alifyatua risasi katika gari la waziri huyo alipokua akikaribia ikulu ya Rais.
    Maafisa wa usalama wanasema kuwa mlinzi huyo alidhani gari hilo lingeleta madhara kiusalama na hakujua kuwa lilikuwa la waziri huyo.
    Rais Mohammed Abdullahi Farmajo ameamuru kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
    Ameahirisha pia safari yake ya kikazi nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria mazishi hayo.
    Abbas alikua mkimbizi katika kambi ya Dadaab na baadae kuwa waziri mdogo zaidi nchini humo huku akihamasiaha raia wengi wa nchi hiyo.

    No comments:

    Post a Comment