• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, May 4, 2017

    WABUNGE WAPIGA KURA ZA NDIO KUFUTA OBAMACARE

    Image result for OBAMACARE
    Utawala wa Rais Donald Trump umekuwa ukishangilia baada ya Bunge la wawakilishi kupitisha muswada uliobatilisha mpango wa afya wa Obamacare ,sheria ya Obama kuhusu gharama nafuu za upatikanaji wa matibabu.
    Mpango huo wa huduma za afya wa Obama ulikuwa ukitoa huduma za bima ya afya kwa mamilioni ya raia wa Marekani, hivyo kutengua mpango huo ulikua moja ya ahadi ya Trump wakati wa Kampeni za urais.
    Muswada huo umepita kwa ushindi mwembamba wa kura 217 kwa 213.
    Muswada huo sasa utapelekwa kwenye bunge la Senate ambao walitoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko ya sheria.
    Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema muswada huo haujulikani utaathiri watu wangapi kutokana na kupoteza bima za afya.
    Haki miliki ya
    Akizungumza baada ya kupigwa kura, rais Trump ameseama ana uhakika muswada huo utapita kwenye bunge la Senate.
    '' kwa miaka miwili nimekuwa nikifanya kampeni na nawaambia kila nilipokuwa nikienda, watu walikuwa wakiathiriaka na mpango huu wa Obamacare, kwa kuwa mimi ninahusika kwenye hili nataka kuwambia kuwa gharama za matibabu zitaanza kushuka, tutahakikisha muswada huu unapita kwenye bunge la senate, nina uhakika''
    upande wa wawakilishi kutoka chama cha Democrat wameeleza madhara ya kura hii iliyopigwa, Steny Hoyer ni mwakilishi ndani ya bunge upande wa walio wachache
    ''wabunge wengi ndani ya bunge la uwakilishi walijua wanaupigia kura muswada mbaya hii leo na Marekani yapaswa kusikitika kwa sababu wabunge wote hawakupiga kura kuipinga, na Marekani itawawajibisha''
    baada ya kura hiyo waandamanaji walikua wakiimba kuonyesha kutounga mkono kura hiyo iliyopitisha muswada huo

    No comments:

    Post a Comment