Kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram,tiktok,youtube n.k ,bila shaka jina la Chief Godlove sio geni masikioni mwao.Amepata umaarufu mkubwa sio tu kama mzalisha maudhui ya mitandao lakini ni Kwa aina ya maisha anayoishi na kushare na watu wengine.
Aina hii ya maisha ya chief Godlove imekuwa ikipokelewa Kwa hisia tofauti tofauti hapa nchini Tanzania.Kijana huyu wa Kitanzania anayejitambulisha kama mfanyabiashara amekuwa akigonga vichwa vya habari mara kwa mara kutokana tu aina ya maisha anayoshare na jamii.Wapo wanaomuona kama ni mtu anayejaribu kuigiza maisha, na mara zote Godlove amekuwa akijibu hilo Kwa kuwaambia wanaosema anaigiza waigize angalau Kwa wiki mbili tu maisha yake.
Pia wapo wanaomuona kama ni mtu anayejaribu kuonesha majigambo dhidi ya masikini. Lakini kwa upande wa tatu wapo wanaomuona kama kijana anayewapa hamasa vijana kupambana na kufikia maisha ya ndoto zao.
Katika makundi hayo matatu mimi nitaangalia zaidi kundi la tatu.
Inawezekana kweli kundi la kwanza na la pili mitazamo yao ikawa ipo sahihi lakini kwa mtazamo wa pili ni lazima kuangalia nguvu ya ushawishi unayoipata kutokana na maudhui ya chief godlove.Inawezekana lugha anayotumia ni lugha ya kukebehi na kuudhi ,lakini hilo lisikufaye ushindwe kuchukua nukta muhimu katika maudhui yake.Pia lazima tujifunze kuambiwa kwa njia kama hiyo kwa maana hata njia za kubembelezwa tulizozizoea hatujawahi kubadilika kwazo.
Kama vijana tunaopambania ndoto zetu hatupaswi kumpuuza kwa kila jambo bali tunapaswa kuamka na hamasa ya juu zaidi katika kubuni, kutekeleza na kuwa imara zaidi ili kufika tunapotaka kufika,wala tusiuone umasikini kama kichaka cha kujificha tusiambiwe kitu chochote bali akili zetu ziamke na kujitafuta zaidi kiuchumi .
Chief godlove pamoja na kutuonesha maisha yake ya kifahari lakini pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia makundi mbalimbali ya wasiojiweza kama watoto yatima, wajane nk, hii inatoa taswira kuu kwamba ana kiu ya kuona vijana wenzake na kila kundi la mtu linaishi katika hali nzuri ya kimaisha.Pia tutambue kuwa wapo watu wengi sana inawezekana wana pesa na utajiri mkubwa kuliko chief godlove lakini hawana moyo wa kuwasanua wengine kuhusu aina ya maisha wanayoishi na kuwatia moyo kwamba wanaweza ikiwa tu watafanya juhudi kutafuta.
Pia amekuwa akiandaa hafla mbalimbali kwa ajili ya kuwahamasisha vijana kupambana kwa bidii na maarifa ili kuondokana na umasikini wa kipato.
Na mwisho kabisa tukumbuke kwamba tuna nafasi ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa na tuondoe nafasi ya kuwachukia waliofanikiwa, Asante.
Imeandikwa na FOL :0783002098
No comments:
Post a Comment