Mahakama ya Rufani ya Tanzania muda mfupi uliopita imefuta rufaa ya kesi ya Uchaguzi iliyofunguliwa na Christopher Chiza dhidi ya Mbunge wa jimbo la Buyungu wilayani Kakonko, mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Bilago Kasuku.
Rufaa hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Christopher Kajoro Chiza baada ya kushindwa katika kesi ya msingi katika Mahakama Kuu mwaka jana. Chiza awali alifungua kesi hiyo ya uchaguzi kupinga Ubunge wa Bilago kwa kile alichodai uchaguzi huo wa ubunge uliofanyika Oktoba 25, 2015 haukuwa huru na haki, huku akiwasilisha vielelezo mbalimbali mahakamani hapo kuonyesha jinsi matokeo ya ubunge yalivyotawaliwa na rushwa, uonevu kwa wananchi na wapiga kura kuanzia kipindi cha kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Afisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema kuwa ushindi huo wa leo ni mwanzo mzuri kuelekea katika kesi nyingine ya rufaa dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu kumvua Ubunge Mbunge wa Longido
"Kwa ushindi huu wa leo imebaki sasa rufaa yetu dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kumvua ubunge Mbunge wetu wa Longido, Mh. Onesmo Ole Nangole. Rufaa yake itasikilizwa Jumatatu ijayo tarehe 14 Agosti 2017 jijini Dar es Salaam" alisema Tumaini Makene
No comments:
Post a Comment