Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeshindwa kutamba mbele ya vijana wenzao wa Cameroon baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa mjini Yaounde, Cameroon.
Kipigo hicho kwa Serengeti Boys ni kisasi baada ya mchezo wa awali kushinda bao 1-0 katika mchezo wa awali ambao ulihudhuriwa na gwiji wa soka Abeid Pelle, Serengeti Boys wapo nchini Cameroon ambako wameweka kambi wakijiandaa na fainali za vijana za Afrika ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Gabon mwezi huu.
No comments:
Post a Comment