|
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo |
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha RPC charles mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi lililosababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu 2 na dereva 1,ambaye pia ndiye mmiliki wa shule ya Lucky Vicent iliyoko kwa morombi jijini arusha.Mkumbo amesema wanamshikilia kwa kosa la kuruhusu basi hilo dogo kubeba abiria zaidi ya uwezo wake.Kwa mujibu wa kamanda mpinga basi hilo lilisajiliwa kubeba abiria 30 tu,lakini siku ya ajali lilikuwa limebeba abiria 38.Mkumbo amesema watamfikisha mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment