• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, May 4, 2017

    JUA IDADI YA WATEJA WA FACEBOOK HADI SASA.

    Image result for FACEBOOK IMAGE
    Faida ya mtandao wa facebook imepanda katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huku mtandao huo ukikaribia kupata wateja bilioni 2 kulingana na ripoti ya matokeo ya mtandao huo.
    Idadi ya watu wanaotumia mtandao huo kila mwezi iliongezeka hadi bilioni 1.94, ambao watu bilioni 1.3 huutumia kila siku kulingana na kampuni hiyo.
    Kampuni hiyo ya Kiteknolojia nchini Marekani iliripoti faida za takriban dola bilioni 3 katika robo ya kwanza ya mwaka ambayo ni ongezeko la asilimia 76 kwa mwaka.
    Hatahivyo imeonya kwamba ukuwaji wa mapato ya matangazo huenda ukashuka.
    Kampuni hiyo pia imepata shinikizo kubwa katika majuma ya hivi karibuni kuhusu vile ambavyo imekuwa ikiangazia maswala ya matamshi ya chuki na unyanyasaji wa watoto.
    Siku ya Jumatano ,Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg alitangaza kwamba atawaajiri watu 3000 zaidi kuweka maudhui ya wastani katika mtandao huo.
    Robo ya idadi ya watu duniani inatumia facebook kila mwezi huku watumiaji wapya wakitoka nje ya bara Ulaya na Marekani Kaskazini.
    Akizungumza baada ya ripoti hiyo ya matokeo ,bwana Zuckerberg alisema kwamba idadi ya watumiaji wake wameipatia Facebook fursa ya kupanua jukumu la mtandao huo ,kuanzisha runinga, afya na siasa.

    No comments:

    Post a Comment