ST.PETERSBURG STADIUM-uwanja huu upo katika kisiwa cha krestovsky.kina uwezo wa kuchukua mashabiki 110,000.uwanja huu ulibuniwa na mjapani aliyeitwa Kisho kurosawa.uwanja huu wenye muonekano wa meli pia una viwanja vya michezo ya kuteleza kwenye barafu.
KALININGRAD STADIUM-uwanja huu uliozingirwa na bustani za kuvutia una uwezo wa kuchukua mashabiki 35,000 pekee.
ROSTOV ARENA-uwanja huu umejengwa takribani mile 20 kutoka katika bahari ya Azov kusini mashariki mwa nchi ya urusi.
FISHT STADIUM-upo katika mji wa SOCHI nchini urusi.ikumbukwe kuwa uwanja huu ndipo zilipofanyika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya olimpic za majira ya baridi mwaka 2014.
LUZHNIKI STADIUM-upo katika jiji la MOSCOW.uwanja huu ulikuwa nimwenyeji wa mashindano ya olimpic mwaka 1980,fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka 2013,pia umewahi kutumiwa na mwanamuziki nguli duniani Michael Jackson alipofanya ziara nchini humo.Hivi sasa unafanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya kutumika kwa kombe la dunia 2018.
VOLGOGRAD ARENA-upo katika mji wa volgograd.uwanja huu umejengwa chini ya mnara wa kumbukumbu ya vita ya pili ya dunia uitwao mamayev kurgan.ulijengwa kuchukua nafasi ya central stadium unaoonekana kulia hapo juu.
SPARTAK STADIUM-upo jijini moscow.uwanja huu pia hujulikana kama "people's team"timu ambayo inasadikiwa haikuwahi kuwa na uwanja wake yenyewe kwa zaidi ya muongo mmoja.katika uwanja huo kuna nakshi za mfano wa dhahabu zenye rangi nyekundu na nyeupe zenye kuwakilisha alama ya spartak na hubadilika rangi zake pale timu ya taifa hilo inapocheza katika uwanja huo.una uwezo wa kuchukua mashabiki 43,298.
NIZHNY NOVGOROD STADIUM-umejengwa katikati ya mito miwili maarufu ya OKAna VOLGA.una uwezo wa kuchukua mashabiki 45,331.
KAZAN ARENA-uwanja huu unafanana kwa kila kitu na viwanja maarufu vya England vya WEMBLEY na EMIRATES STADIUM kinachomilikiwa na klabu ya Arsenal.pia mbele ya uwanja huo kuna screen kubwa yenye kuchukua eneo la mita 3700 na ndio kubwa zaidi duniani.ulizinduliwa mwaka 2013 na umekuwa ukitumika katika ligi kuu nchini urusi.
MORDOVIA ARENA-kipo katika mji wa saransk na kina uwezo wa kuingiza mashabiki 44,442.ni kiwanja kipya kinachotarajiwa kukamilika mwa huu 2017.
No comments:
Post a Comment