• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Tuesday, May 16, 2023

    WATUMISHI NATTA WAPONGEZWA KWA UCHAPAKAZI


    Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Tusekile Benard akizungumza na Watumishi wa kata ya Natta katika sherehe ya Mei Mosi 2023 iliyofanyika katika ukumbi wa Nyitika Lodge-Natta.

     Watumishi wa kata ya natta wamepongezwa Kwa juhudi zao ambazo zimeifanya kata hiyo kuwa na sifa nzuri katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti.Akizungumza na watumishi wa kata hiyo afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Tusekile Benard Mwakeja ambaye alikuwa mgeni rasmi amewapongeza watumishi wa idara zote ndani ya kata Kwa kufanya kazi Kwa juhudi na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sehemu zao za kazi.Miongoni mwa changamoto hizo ni uhaba wa watumishi,upandishwaji wa madaraja Kwa watumishi Pamoja na miundombinu.

    Afisa mtendaji wa kata ya Natta bwana Sagenda Bomani aliwataka watumishi kuendeleza umoja uliopo kwani unaleta chachu katika utendaji Pamoja na kusaidiana katika matatizo mbalimbali.Pia bwana Sagenda alisisitiza juu ya wajibu walionao watumishi katika kuisaidia serikali kuleta maendeleo na ustawi wa taifa.

    Akizungumza na watumishi diwani wa kata ya natta Juma porini Keya amewataka watumishi kuzingatia Sheria za utumishi na kuwataka viongozi kuacha kuwatishia watumishi Kwa kutumia nafasi zao badala yake waweke mazingira rafiki ya kuwapa motisha watumishi Ili wachape kazi Kwa bidii zaidi.

    Sherehe ya mei mosi kata ya Natta iliandaliwa na kuratibiwa na ofisi ya mtendaji wa kata yaNatta Kwa kushirikiana na kamati ya maendeleo ya kata WDC Kwa lengo la kuwapongeza watumishi ndani ya kata ya Natta Kwa kazi nzuri wanazofanya.

    Katika sherehe hiyo taasisi mbalimbali zilitunukiwa vyeti vya pongezi Kwa kufanya vizuri zaidi.Kwa upande wa afya kituo Cha afya natta kilipata cheti Cha pongezi Kwa kuimarisha mfumo wa ukusanyaji mapato na kuboresha huduma za afya.Pia katika sekta ya elimu shule kadhaa zilitunukiwa vyeti Kwa kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la Saba 2022,shule hizo ni shule ya msingi Nattabigo,shule ya msingi Motukeri na shule ya msingi Makundusi.Kwa upande wa sekondari shule ya sekondari Natta ilitunukiwa cheti Cha pongezi Kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato Cha sita 2022,na shule ya sekondari Makundusi ilitunukiwa cheti Cha pongezi Kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato Cha nne 2022.


    Imeandikwa na 

    Mwl.Frank O Lungwa.+255783002098





    No comments:

    Post a Comment