Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kupatikana kwa amani mashariki ya kati katika mazungumzo na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.
Katika taarifa ya pamoja waliotoa kwa vyombo vya habari rais Trump aliapa kwamba ''tutahakikisha hili linatendeka''.
Bwana Abbas alimuambia Trump katika ikulu ya Whitehouse kwamba anataka kuwepo kwa makubaliano ya amani ya mpango wa kudumu wa mataifa mawili yalio huru ikiwemo mipaka iliokuwepo kabla ya 1967.
''Sasa rais tuna matumaini na wewe'',alisema bwana Abbas.
Hatahivyo bwana Trump amekuwa na mawazo tofauti kuhusiana na utatuzi wa mataifa mawili yalio huru.
No comments:
Post a Comment