FAHAMU ROUTERS NA KAZI ZAKE
Ninapozungumzia router hautakuwa msamiati mgeni kwa wale wanaosoma kozi za networking pamoja na wale wanaofanya kazi zihusianazo na mtandao wa kompyuta.Router ni kifaa cha mtandao ambacho kina uwezo wa kuunganisha mtandao mmoja na mwingine,kwa kifupi unapotaka kuunganisha mitandao miwili tofauti ya kompyuta utalazimika kutumia kifaa hiki.
Inawezekana moja kwa moja ninapozungumzia mtandao wengine wakaunganisha moja kwa moja na intaneti lakini ukweli unabaki kuwa pale pale kwamba intaneti ni sehemu tu ya mtandao.
Kwa leo nitakihusianisha kifaa hiki cha kimtandao na aina ya mtandao iitwayo LAN,mtaniwia rdhi kwa sababu sifahamu jina lake kwa lugha ya kiswahili.LAN ni kifupisho (abbriviation)cha maneno Local Area Network.Aina hii ya mtandao huhusisha kushare baadhi ya data kutoka kompyuta moja kwenda nyingine ndani ,aidha ya jengo dogo au chumba.(within a single building).LAN itawezesha kompyuta zilizounganishwa kwa kutumia waya maalumu za kopa ( copper cable)twisted pair,aidha ni cat5 ,cat6 na nyinginezo.
Njia hii ya kutengeneza mtandao huhitaji anuani maalumu za kompyuta(ip address)ili kuleta mawasiliano sawia kwa kopyuta husika.Hapa mnaweza kushare jumbe mbalimbali,kutuma na kupokea data kutoka komputa moja kwenda nyingine nk.
inapotokea kuna LAN zaidi ya moja ,aidha ndani ya jengo husika au nje ya jengo hilo basi LAN hizo ni lazima ziunganishwe na kifaa hiki kiitwacho router.Inawezekana LAN moja ipo katika ofisi kama hiyo Dodoma na nyingine ipo Mwanza na wanataka kushare taarifa kupitia hizo LAN,basi router ndio hufanya kazi ya kuziunganisha hizo LAN.
Si hivyo tu,Router pia inaweza kutumika kupata huduma ya intaneti kwa LAN husika kama ikibidi ,ila kwa huduma ya intaneti itabidi ofisi husika kupata huduma hiyo kupitia kwa watoa huduma za intanet yaani internet service privider(ISP)
Ikumbukwe pia kuwa zoezi hili lote linahitaji kufanywa na wataalamu wenye ujuzi (network engeneers)ambao watafanya configuration kwa ajili mtandao wako ikiwemo maswala ya kiusalama wa mtandao wako nk.
Hiyo ndio router
Tukutane katika makala nyingine ya technolojia ambapo nitakuletea maelezo ya kina kuhusu SWITCH na namna inavyofanya kazi kwa kushurikiana na ROUTER.

No comments:
Post a Comment