• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Saturday, January 28, 2017

    NIMEKUSOGEZEA TOP 5 YA VIWANJA VYA NDEGE VIKUBWA ZAIDI ULIMWENGUNI

    1-KING FAHD INTERNATIONAL AIRPORT-                                                                                 Upo kilometa 20 kaskazini mashariki mwa mji wa DAMMAM katika nchi ya Saudi Arabia.Una ukubwa wa hekta 77600.Uwanja huu wa ndege ulizinduliwa rasmi mwaka 1990 na ndio mkubwa kuliko viwanja vya ndege vyote hapa duniani.

    2-DENVER INTERNATIONAL AIRPORT-

    Una ukubwa wa hekta 13,726.Upo katika nchi ya Marekani.Hutumiwa na abiria takribani 31 milioni kwa mwaka,huku kukiwa na wastani wa safari za ndege zipatazo 635,445 kwa mwaka.Uwanaja huu wa ndege ndio mkubwa Zaidi katika nchi ya Marekani.
     

    3-DALLAS INTERNATIONAL AIRPORT-
    una ukubwa wa hekta 7800.Upo katika mji wa DALLAS nchini Marekani.Una vituo vya ndege (terminals)5 huku kukiwa na mageti 165.Pia uwanja huu una uwezo wa kupanuliwa na kujengwa vituo vya ndege(terminals)13 na mageti 260.




    4-SHANGHAI PUDONG INTERNATIONAL AIRPORT
    Una ukubwa wa hekta 3350 upo nchini China .Unatumiwa na abiria 51,661,800 kwa mwaka.



    5-CHARLES DE GAULE AIRPORT
    una ukubwa wa hekta 3200.Uwanja huu upo kaskazini Mashariki mwa jiji la Paris nchini ufaransa.unatumiwa na abiria wapatao 62,052,917 kwa mwaka,katika safari za wastani wa 497,763 zinazofanyika uwanjani hapo kwa mwaka.


    Na Frank Lungwa


    No comments:

    Post a Comment