• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Sunday, May 7, 2017

    WASICHANA 80 WA CHIBOK WAACHILIWA HURU NIGERIA


    Image result for chibok girls
    Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa 2014, wameachiwa huru.
    Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.
    Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria
    Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon.

    No comments:

    Post a Comment