• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Tuesday, April 9, 2024

    HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YAKAMILISHA MAFUNZO YA WALIMU MAHIRI KWA MAFANIKIO

     HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YAKAMILISHA MAFUNZO YA WALIMU MAHIRI KWA MAFANIKIO


    Natta, Serengeti.

    09 April 2024

    Halmashauri ya wilaya ya serengeti,Mkoani mara imekamilisha mafunzo kwa walimu mahiri  ndani ya wilaya ya Serengeti kwa mafanikio makubwa.Mafunzo hayo yaliyolenga kuwanoa walimu ili kuendana na mabadiliko yaliyopo katika mtaala wa elimu ya msingi ulioboreshwa mwaka 2023.Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na walimu maalumu 42 ambao walipata mafunzo ya uwezeshaji yaliyofanyika wilayani Bunda,yamefanikiwa kwa kuwafikia walimu wote ndani ya wilaya ya Serengeti.

    Mafunzo haya yaliyofanyika  kwa siku moja katika kanda tano yalisimamiwa na waratibu elimu kata ambao walifanya kazi kubwa kuhakikisha mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ufanisi.

    Akizungumza na walimu katika kituo cha mafunzo cha shule ya msingi  Nattabigo afisa elimu wilaya ya Serengeti Bw. Mujibu Babara amewapongeza walimu kwa kujtolea na kushiriki kupata mafunzo hayo kwani yataleta chachu katika swala la ufaulu wa wanafunzi katika wilaya ya Serengeti na mkoa kwa ujumla.Bw.Babara aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha walimu kuandaa na kufanya tathmini kwa wanafunzi kwa kuzingatia maboresho ya mtaala unaotumika sasa.

    Aidha Bw.Babara amewataka walimu kujitolea na kufanya kazi kwa uzalendo na kuacha alama za utendaji kazi uliotukuka katika maeneo yao ya kazi.

    Pia afisa elimu taaluma wilaya Serengeti Bw.Msabaha alitoa tathmini ya hali ya elimu kiwilaya kuwataka walimu wa masomo ya hisabati na english kuongeza juhudi zaidi kwani masomo hayo yameonekana kuwa na ufaulu wa kiwango cha chini ukilinganisha na masomo mengine.Pia amewataka walimu kufanya tathmini na upimaji kwa kuzingatia mafunzo waliyoyapata.


    Imeandikwa na Frank Lungwa

    lungwafrank2017@gmail.com

    Whatsapp: +255783002098

    l






    2 comments:

    1. Asante kwa kutuhabarisha

      ReplyDelete
      Replies
      1. Tinashukuru Sana Kwa mrejesho wako,endelea kuwa karibu nasi

        Delete