• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, June 1, 2017

    IS NA TEKNOLOJIA

    Kundi la Islamic State militant (IS) linapigana vita vyake kwa njia mbali mbali dhidi ya wale wanaotaka kulishinda. Moja wapo ya vita vyake ni vya njia ya digitali.
    IS mara nyingi hutumia vita vya vyombo vya habari sambamba na ile ya ardhini na mara nyingi ''wafia habari" - watu wanaokufa wakati wapokuwa wakitengeneza kanda za video na picha nyingine za digitali kwa ajili ya kundi hilo.
    Kama ilivyo kwa makundi kama hilo, IS limekuwa mstari wa mbele katika matumizi ya mitandao ya habari ya kijamii na wavuti, kutangaza propaganda juu ya mafanikio yake na kuvitumia kama chombo cha kuwaingiza kwenye kundi hilo wafuasi wapya.
    Licha ya kwamba kundi hilo ni mtumiaji wa muda mrefu wa mitandao ya kijamii ya habari, shughuli za IS zilichukua mkondo mpya mwezi Septemba 2015 wakati vyombo vyake vya habari vilipoingia kwenye mfumo wa programu ya ujumbe wa Telegram.
    Hatua hiyo ya kutumia huduma ya ujumbe ilikuja baada ya kuwa na mzozo wa muda mrefu na Twitter, ambayo mara kwa mara imekuwa ikifunga akaunti za IS, na baadhi ya majaribio kadhaa ya IS ya kutumia Twitter zisizokuwa na utambulisho yalifungwa pia.
    Nembo rasmi ya IS , Nashir, ( kushioto) na nembo ya shirika la habari la Nashir (kulia)Haki miliki ya picha NASHIR/NASHIR NEWS AGENCY
    Image caption Nembo rasmi ya IS , Nashir, ( kushioto) na nembo ya shirika la habari la Nashir (kulia)
    Kuanzishwa kwa programu ya ujumbe ya Telegram kulikuja wakati muafaka ambapo Telegram ilibuni "muundo" ambao uliwapatia fursa watumiaji kutangaza kwa idadi ya watu isiyo na kikomo - mfumo ambao makundi mengi ya jihadi ya mtandaoni yaliharakisha kuutumia.
    Hatua hiyo ilitambuliwa na Telegram, na IS walitoweka kwenye mfumo huo mwezi Agosti 2016 baada ya akaunti yake rasmi kufutwa mara mbili.
    Lakini vyombo vya habari vya IS hutoa taarifa kupitia vyombo tofauti ambavyo huonekana kurudia matangazo yanayoyaonekana kwenye vyombo rasmi vya habari vya kundi hilo.
    Miongoni mwa vyiombo rasmi vya habari vya kundi hilo ni pamoja shirika la habari la Amaq, na shirika hilo linaelezewa kama shirika lililojitolea kugawa taarifa rasmi za IS.
    Hii huliwezesha kundi la IS kuvutia idadi kubwa ya wafuasi , lakini kwa kawaida matangazo hayo huondolewa kabla ya kuzidi 1,000.
    Idadi hiyo ya ujumbe inatosha kuiwezesha IS kusambaza ujumbe kwa wafuasi wake wa mtandaoni.
    Takwimu maarufu zinazoegemea upande wa -IS hueneza moja kwa moja propaganda zake sambamba na taarifa nyingine.

    No comments:

    Post a Comment