Watu wasiopungua 8 wameuliwa na wengine 4 wamejeruhiwa Alhamisi wakati gari moja lililojaa milipuko ilipogonga kituo cha polisi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Ripoti ya VOA imeeleza kuwa shambulio hilo lililenga kituo cha Polisi cha Waberi kwenye bara bara iliyoko eneo la Makaramah yenye shughuli nyingi.
Mwandishi wa VOA Somalia amesema alimuona mtu aliyekuwa akiendesha Toyota Surf akiongeza kasi kuelekea kituo cha polisi.
Timu ya waokowaji walikuwa kwenye eneo la tukio kusaidia waliojeruhiwa.
Hakukuwa na madai ya kuhusika lakini kundi la wanamgambo la al-Shabab kawaida linashambulia majengo ya serikali na maeneo ambayo maafisa wa serikali wanakutana kila wakati.

No comments:
Post a Comment