• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, June 22, 2017

    ZUMA KIKAANGONI TENA KATIKA KURA YA SIRI


    Image result for jacob zuma

    Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imeamuru kuwa kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma inaweza kufanywa kwa siri.
    Mahakama ya katiba ilisema kuwa spika wa bunge na haki ya kuamuru hatua kama hiyo. Awali alisema kuwa hakuwa na mamlaka kama hiyo.
    Vyama vya upnzani vinaamini kuwa chini ya kura ya siri, wabunge kutokla chama cha Zuma cha ANC wanaweza kupiga kura ya kumpinga.
    Zuma aliponea kura za awaliaza kutokuwa na im,ni naye.
    Bwana Zuma amekuwa chini ya shinikizo kufuatia shutuma nyingi ikiwemo madai ya ufisadi na mabadiliko kwa baraza la mawaziri yaliyokumbwa na utata.
    Akitoa uamuzi huo Jaji mkuu Mgoeng Mgoeng, alisema kuwa spika wa bunge ana mamlaka ya kuamua ni njia gan kura hiyo itafanyika.
    Spika wa bunge Baleka Mbete ni afisa wa cheo cha wa ANC na alikuwa amedai kuwa sheria za bunge haziruhusu kufanyika kura ya siri,
    Sasa tarehe mpya ya kura hiyo ya kutokuwa na imani itatangazwa.

    No comments:

    Post a Comment