• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Saturday, June 24, 2017

    Matokeo ya urais kutangazwa rasmi bungeni:Kenya.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Bw. Chebukati
     Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Bw. Chebukati anasema tume hiyo imejiandaa vyema kwa zoezi la uchaguzi 
                  
    Mahakama ya Rufaa imeamua matokeo rasmi ya kura za urais yatatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi vituo vya kuhesabu kura kwenye maeneo bunge.
    Uchaguzi wa Kenya utafanyika tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu ambapo Rais Uhuru Kenyatta atang'ang'ana kuhifadhi wadhifa wake dhidi ya mpinzani wake wa jadi Raila Odinga
    Uamuzi huo wa majaji watano wa Mahakama ya Rufaa umeonekana kama ushindi mkubwa kwa muungano wa upinzani.
    Jopo la majaji watanao limesema kwamba mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC hana mamlaka kisheria ya kuhakiki na kutangaza matokeo ya urais.
    Wakenya wakiwa kwenye foleni za kupiga kura
     Wakenya wakiwa kwenye foleni za kupiga kura
    Msimamo wa tume ya uchaguzi, ni kwamba lazima maafisa wake wahakiki matokeo yote kutoka maeneo bunge katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura, na kwamba wana uwezo wa kubadilisha matokeo hayo.
    Serikali ilikuwa inaunga mkono msimamo huo, japo upinzani ulipinga.
    Kwa muda mrefu upinzani umekuwa ukieleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa muungano tawala kushirikiana na tume ya uchaguzi kuhujumu matokeo ya uchaguzi.
    Tume ya uchaguzi imekana madai hayo.
    Uchaguzi wa agosti 8, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga.
    Mahakama hiyo pia ilisema mahakama ya juu ina uwezo wa kisheria wa kutatua mizozo inayotokana na uchaguzi wa urais.

    No comments:

    Post a Comment