• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Saturday, June 24, 2017

    Mauricio ateuliwa meneja wa Southampton

    Mauricio Pellegrino
    Pellegrino (kulia) aliteuliwa meneja wa Alaves Juni 2016 baada ya klabu hiyo kupandishwa ngazi kucheza La Liga
    Southampton wamemteua Mauricio Pellegrino kuwa meneja wao mpya.
    Raia huyo wa Argentina wa miaka 45, amechukua nafasi ya Claude Puel, aliyefutwa kazi mapema mwezi huu baada ya kuwa kwenye usukani kwa msimu mmoja.
    Pellegrino alijiuzulu wadhifa wake kama meneja wa klabu ya Alaves ya Uhispania mwishoni mwa Mei, baada ya kushindwa fainali ya Kombe la Uhispania na Barcelona na kusaidia klabu hiyo kumaliza nafasi ya tisa La Liga. Alikuwa amesaidia klabu hiyo kupanda daraja msimu uliotangulia.
    "Filosofia yangu na utamaduni wa klabu hii vitaendana vyema sana," amesema Pellegrino ambaye ametia saini mkataba wa miaka mitatu.
    "Ninataka kushinda mechi, kufanikiwa na kuendeleza moyo wa kufanya kazi kama timu ambapo kila mmoja anajitolea 100% na kusaidiana.
    "Nina furaha sana na nina matumaini kuhusu siku zijazo."
    Pellegrino awali alifanya kazi klabu za Independiente na Estudiantes nchini Argentina, ambapo alijiunga na Estudiantes baada ya kufutwa kazi na Valencia - kazi yake ya kwanza kama maneja - baada ya kuwa kwenye usukani miezi saba.

    Kabla ya kupewa kazi Alaves Mei 2012, Pellegrino alifanya kazi kama mmoja wa wakufunzi wa Rafael Benitez katika Liverpool (2008-2010) na Inter Milan (2010).
    Kama mchezaji, alichezea Liverpool mechi 15 mwaka 2005 baada ya kununuliwa na Benitez ambaye alikuwa amecheza chini yake kwa miaka sita Valencia tangu 1999.
    Puel alikuwa meneja wa tatu kuiaga Southampton kwa miaka mitatu iliyopita, baada ya Mauricio Pochettino kuhamia Tottenham na Koeman kuelekea Everton.
    Meneja huyo wa zamani wa Monaco alipigwa kalamu mwaka mmoja baada ya Koeman kuiaga klabu hiyo mwezi Juni mwaka 2016.

    No comments:

    Post a Comment