Takriban watu 45 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye hoteli inayoandaa mkutano wa afya kwenye mji mku wa Kenya Nairobi.
Maafisa wanaonya kuwa huenda idadi ya walioambukizwa ikaongezeka. Wanasema kuwa wale wote walioambukizwa ugonjwa huo wamelazwa hospitali moja mjini Nairobi.Chanzo cha ugonjwa huo bado hakijulikani lakini mara nyingi husambaa kwa njia ya chakula na maji.
Mwezi uliopita watu watano walikufa kutokana na ugonwa wa kipindupindu na kulazimu utawala kuweka vituo vya ukaguzi kote mjini Nairobi
No comments:
Post a Comment