Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini jana usiku ametoa hotuba kupitia televishani huku akitangaza kujiuzulu mara moja.
Kwenye hotuba yake ya dakika 30, amesema kuwa ingawa sikubaliani na uamuzi wa kamati ya utendaji ya chama tawala cha Afrika Kusini ANC ambao unamtaka kuondoka mara moja, lakini chama hicho cha ANC hakiwezi kutenganika kutokana na mimi. Hivyo naamua kujiuzulu mara moja.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, baada ya kujiuzulu kwa rais Zuma, mwenyekiti mpya wa chama cha ANC ambaye pia ni makamu wa rais Bw. Cyril Ramaphosa atakuwa kaimu rais wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment