Mahakama ya kijeshi nchini Somalia, imemhukumu mtu mmoja adhabu ya kifo kwa kutekeleza shambulio mbaya zaidi nchini humo, mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Hassana Adan Isaq alishutumiwa kwa kuongeaza kundi dogo la al-Shabaab liliotekeleze shambulio hilo.
Wakati kesi ilipokuwa inasikilizwa , kijana huyo wa miaka 23 alikataa uhusiano na tukio hilo.
Watu wengine wawili walipatikana na hatia kwenye kesi hiyo na wamepewa adhabu ndogo.Mmoja alipewa hukumu ya kufungwa jela miaka mitatu.
Lori moja lililokuwa limejazwa vilipuzi, lililipuka nje ya hoteli moja mjini Mogadishu Oktoba mwaka jana wa 2017 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 500.
Ni jambo nadra sana kuona uchunguzi mkubwa kama huu kupelekea kwa mtuhumiwa kuhukumiwa kwa shambulio nchini Somalia, amesema mwandishi wa masuala ya Usalama, Tomi Odalipo.
Anasema shambulio hilo lilipelekea hisia nyingi za hasira kutoka kwa umma dhidi ya al- Shabaab kwa inayoaminika kuwa uhusiano wao na shambulio hilo na pia dhidi ya serikali lililokosa kuzuia shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment