• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Saturday, July 8, 2017

    Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya afariki dunia

    Meja mstaafu Joseph Nkaissery, aliaga dunia Jumamosi  asubuhi katika hospitali ya Karen, kilomita chache kutoka mjini Nairobi

    Image result for Joseph Nkaissery
    Afisa mmoja katika ikulu ya Nairobi ambaye hakutaka jina kale litajwe kwa sababu hana idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari aliiambia Sauti ya Amerika kwa njia simu kwamba Nkaissery alikuwa ameenda hospitalini ili kukaguliwa na madaktari na wauguzi.
    Hata hivyo, hakutoa habari zaidi juu ya kile kilichosababisha kifo chake.
    Baadaye, afisa mwandamizi katika ikulu, Joseph Kinyua, alitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kuthibitisha kifo cha waziri huyo.
    Kabla ya kulalamika kwamba hakuwa anajihisi vizuri, Nkaissery alikuwa ameandamana na rais Uhuru Kenyatta wakati wa mkutano wa maombi ya kitaifa uliofanyika kwenye bustani za Uhuru Park Ijumaa.
    "Alionekana mwenye afya lakini baadaye akasema alihitaji kwenda hospitalini kwa ukaguzi," mtu mmoja ambaye hakutambulishwa, amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema.
    Aliteuliwa kama waziri wa uslama wa ndani mnamo tarehe 2 Desemba 2014, kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Joseph Ole Lenku.
    Kabla ya uteuzi huo, alikuwa mbunge wa chama cha upinzani, ODM, akiwakilisha eneo bunge la Kajiado ya Kati.
    Amefariki akiwa na umri wa miaka 68.

    No comments:

    Post a Comment