• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Monday, July 17, 2017

    FAHAMU AIRPLANE MODE NA FAIDA ZAKE KATIKA SIMU YAKO


    Image result for AIRPLANE MODE
    Airplane mode ni mfumo uliopo katika vifaa vya mawasiliano hasa katika simu zetu mpanguso(janja)pamoja na tablets.Inawezekana umewahi kujiuliza kuwa ni nini hasa matumizi ya mfumo huu hasa kuangazia faida zake kwa watumiaji wa vifaa vya mawasiliano.

      Kama ilivyo kwa jina lenyewe la mfumo airplane,huwakilishwa na alama ya ndege inayopaa.Mfumo huu unapokuwa umewashwa kwenye kifaa chako cha mawasiliano huzima mifumo yote ya kiredio inayojumuisha,bluetooth,wifi pamoja na mitandao ya simu)Radio ni aina ya technolojia ya mawasiliano ambayo hutumika kusafirisha na kupokea mawasiliano katika vifaa mbalimbali vya mawasiliano.Technolojia hii ipo sambamba na technolojia nyingine hasa zile za huduma za mtandao wa internet kwa kutumia fibber au copper.

      Kwa kifupi airplane mode hutumika kama switch ya kuzima na kuwasha huduma zote hizo za mitandao ya simu,bluetooth na wifi kwa wakati mmoja.Kwa lugha nyingine ukiwasha mfumo wa airplane mode hutoweza kupata huduma za mitandao ya simu,bluetooth na wifi.

       Huduma hii iliwekwa mahususi kwa watu walio katika safari ya ndege ili waweze kutumia simu zao kwa huduma nyingine bila kulazimika kuzima kabisa simu zao.Hii inaa maana kwamba abiria wa ndege ataweza kutumia huduma  kama kupiga picha kwa kutumia kamera ya simu yake,kusikiliza muziki na video zilizohifadhiwa katika simu yake na huduma nyingine isipokuwa zile nilizozitaja hapo juu yaani kufanya mawasiliano ya simu,kushare kwa bluetooth,wifi na hata huduma ya GPS.

    kwa nini airplane mode kwenye ndege.

    Ili simu iweze kupata mawasiliano hutuma ishara kila wakati ili kutafuta mnara wa mawasiliano husika,hivyo kitendo hiki kinaweza kuingiliana na mawasiliano ya ndege na hivyo kuweza kusababisha rubani kushindwa kumudu kuiongoza ndege husika. Pamoja na hili,technolojia huvumbuliwa kila siku kukabiliana  na changamoto mbalimbali,kwani kwa sasa kuna baadhi ya ndege ambazo huruhusu huduma za wifi ndani ya ndege ,na hii ni kutokana na vifaa maalumu ambavyo hufungwa kwenye ndege ili kuepusha mwingiliano kati ya mawasiliano ya ndege na vifaa vingine vya mawasilano.
                                                    
                                                   faida za kutumia huduma hii
    Kama utaamua kuitumia huduma hii hata kama sio kwenye ndege,itakusaidia kukifanya kifaa chako kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi,kwani kitendo cha simu kutafuta ishara kila wakati huigharimu simu chaji nyingi sana.

    UNA MAONI AU USHAURI KUHUSU KIFAA CHAKO CHA MAWASILIANO ? NIACHIE UJUMBE HAPO CHINI.

    imeandaliwa na Frank Lungwa

    No comments:

    Post a Comment