• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Tuesday, July 4, 2017

    MAREKANI YAFANYA SHAMBULIZI LA ANGA SOMALIA

    Image result for us air force

    Marekani imefanya shambulizi la angani huko Kusini mwa Somalia Jumapili jioni, Kikosi cha US Africa command kimeiambia VOA.
    Kikosi hicho hakikuelezea nani aliyekuwa amelengwa na shambulizi hilo lakini kimesema kinafanya tathmini ya athari za operesheni hiyo.
    Wakati huohuo, vyanzo vya usalama kusini mwa Somalia vimeiambia VOA kuwa shambulizi hilo lililenga magari yaliokuwa yanawasafirisha maafisa wa Al-Shabab katika eneo la mji wa Kunyo Barrow eneo la chini ya mkoa wa Shabelle jioni Jumapili.
    Afisa wa ngazi ya juu wa usalama ambaye jina lake halikuweza kutajwa ameiambia VOA kuwa shambulizi hilo liliharibu magari na kuuwa watu waliokuwa ndani yake.Ofisa huyo amesema kuwa waliolengwa ni wafuasi wa Al-Shabab ambao wako kwenye kikundi kilichokuwa na tawi lake Puntland ambalo linapigana dhidi ya vikosi vya eneo katika milima ya Galgala.
    Al-Shabab hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya kinyama katika kambi ya jeshi la Somalia kwenye eneo la Af-Urur, Puntland, na kuwaua takriban wanajeshi 50 wa serikali katika mkoa huo.
    Hii ni mara ya pili Marekani inawalenga wapiganaji wa Al-Shabab tangia Rais Trump aingie madarakani.
    Mnamo Juni 10, Shambulizi la Marekani liliuwa wapiganaji wa Al-Shabab karibu na mji wa Saakow ulioko katika mkoa wa kati wa Jubba.

    No comments:

    Post a Comment