• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, July 6, 2017

    MKANYAGANO WASABABISHA VIFO VYA MASHABIKI WA KANDANDA 8

    Watu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi
    Image captionWatu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi
    Watu wanane wakiwema watoto saba wameuwawa kwenye mkanyagano kabla ya kufanyika kwa mechi ya kandanda nchini Malawi.
    Watu wengine zaidi walijeruhiwa wakati wa mkanyagano huo ulitokea uwaja wa Bingu mjini Lilongwe.
    Mkanyagano huo unaripotiwa kutokea wakati maefu ya watu walijaribu kutafuta viti kabla ya mchuano wa kirafiki kati vilabu vikubwa vya Nyasa Big Bulets na Silver Strikers.
    Rais Peter Mutharika ametuma rambi rambi zake na kusema kuwa serikali inafanya kila iwezalo kuzisadia familia za waliouawa.
    Mwandishi wa BBC aliye Malawi anasema kwa milango ya uwanja huo unaowachukua watu 40,000 ilistahili kufunguliwa kuruhusu watu kuingia mapema lakini ilichelewa kwa muda wa saa tatu.
    Hata hivyo maelfu walikwa wamefika na baadhi walijaribu kuingia kwa nguvu hali iliyosababisha polisi kufyatua vitoa machozi.
    Inspekta wa polisi aliliambia shirika la Reuters kuwa anatarajia idadi wa waliokufa kuongezeka.

    No comments:

    Post a Comment