• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Friday, July 7, 2017

    NIMEKUSOGEZEA HII,MWANAMKE ALIEIKOJOLEA BENDERA YA MAREKANI


    Emily Lance alitengeza video akiikojolea bendera ya Marekani
    Mwanamke aliyesambaza kanda yake ya video akiikojolea bendera ya Marekani ametoa wito kwa watu kutoilenga familia yake akisema hawaungi mkono tendo lake.
    Emily Lance alipokea vitisho vya mauaji katika mtandao wa kijamii na ubakaji baada ya kuchapisha kanda hiyo ya video siku ya uhuru wa taifa hilo.
    Akaunti yake haiko tena katika mtandao wake wa facebook lakini awali alikuwa amechapisha kwamba babake na eneo analofanya kazi pia limelengwa, kulingana na ripoti.
    Kutoheshimu bendera ya Marekani sio kinyume cha sheria kutokana na sheria nyingi na uhuru wa kujieleza.
    Katika kanda hiyo ya video, Bi Lance anaonekana akisimama juu ya choo ambapo bendera ya Marekani imewekwa na kuikojolea kupitia usaidizi wa chombo ambacho kinawasaidai wanawake kufanya hivyo wakiwa wamesimama.
    Chini yake aliandika maneneo ya kuitusi bendera hiyo.
    Baadaye aliwataka wanaopinga wazo lake kutowalenga watu wasio na hatia akisema hakuna hata mtu mmoja katika familia yake anayeunga mkono wazo lake.

    No comments:

    Post a Comment