Hatimye kitendawili cha wanachuo wa UDOM wa kozi ya ualimu wa masomo ya Sayansi ,hisabati na teknolojia zaidi ya 7802 waliofukuzwa wiki iliyopita,kimeteguliwa leo na rais wa jamhuri ya muungano wa Tazania.
Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msing la maktaba ya kisasa kabisa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam uliofadhiliwa na serikali ya China,Rais John Pombe Joseph magufuli amesema kuwa wanachuo hao hawana vigezo vya kuwepo chuoni hapo.Aidha rais amesema kuwa wanafunzi hao walipaswa kusoma katika vyuo vya ualimu vilivyopo nchini ambavyo kwa sasa vina upungufu wa wanafunzi.Magufuli amesema Diploma waliyokuwa wakisoma katika chuo cha Udom inatolewa pia na vyuo vingine vya ualimu.
Aidha rais magufuli amesema kuwa wanachuo waliofukuzwa wenye ufaulu wa daraja la kwanza na la pili ,serikali itaangalia namna ya kuwasaidia lakini wenye ufaulu chini ya hapo waangalie utaratibu mwingine wa kujisomesha.
Pia katika hafla hiyo rais Magufuli ametoa sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa chuo hicho.Aidha rais magufuli amewashauri wawekezaji wengine kuwekeza katika kujenga makazi katika vyuo vilivyopo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment