• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Sunday, June 19, 2016

    CHUO CHA MADINI ARUSHA CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA KWANZA.

        Chuo cha madini cha Arusha kimefanya mahafali yake ya kwanza hapo jana tar 18/09/2016.Katika mahafali hayo wanafunzi kumi walikuwa wakihitimu masomo yao katika ngazi ya cheti.Mahafali hayo yaliyohudhuriwa na idadi ndogo ya watu,mgeni rasmi alikuwa ni kamishna wa madini mkoa wa Arusha.
    kamishna wa madini mkoa wa Arusha(katikati waliokaa)akiwa na baadhi ya wakuu wa vyuo mkoani Arusha.Kushoto kwake ni mkuu wa chuo cha madini Arusha,bw Emmanuel Lukumai
      Akisoma risala iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya wahitimu na uongozi wa chuo mkuu wa chuo cha madini Arusha bw Emmanuel lukumai amesema chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa majengo jambo linalofanya chuo kutumia fedha nyingi katika ulipaji wa pango.Pia katiaka mafanikio ambayo chuo hicho kimepata bwana lukumai amesema tokea kuanzishwa kwa chuo hicho kumekuwa na mafanikio kadhaa ikiwemo wanafunzi wa chuo hicho kuajiriwa sehemu mbalimbali nchini.Pia katika mahafali hayo kulifanyika maonyesho maalumu ya madini mbalimbali.
         Ili kukabiliana na tatizo la ajira,chuo cha mdini Arusha kimeanzisha utaratibu wa kuwa na saccos kwa wahitimu kila mwaka ambayo itawasaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kumudu gharama za kukata madini na kuyauza.Katika kufanikisha hilo ,kamishna wa madini ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi ,alizindua saccos iliyopewa jina la TANZANITE PRE- COOPERATIVE GROUP na kufanya harambee iliyokusanya takribani shilingi 3,572,000. ikiwemo fedha taslimu pamoja na ahadi.
    Baadhi ya wahitimu wa chuo cha madini Arusha

    Mahafali hayo yalifanyika katika Jengo la CCM lililopo sanawari mkoani ARUSHA.

    imeandikwa na frank Lungwa.

    No comments:

    Post a Comment