Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF prof.Ibrahim haruna Lipumba ,ambaye alijiuzulu wadhifa wake wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu mwaka jana ,amerudi tena katika chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CUF jijini Dar es salaam,lipumba amesema kuwa amemuandika barua katibu mkuu wa chama hicho kuomba atengue barua yake ya kujizulu aliyoiandika mwaka jana.Akizungumza kwa masharti ya kutohojiwa swali lolote ,Lipumba amesema ameamua kurudi katika siasa kutokana na ubakaji wa demokrasia unaoendelea hapa nchini.Hata hivyo kurudi kwake rasmi kunategemea uamuzi utakaotolewa na chama hicho mara baada ya kupitia barua yake kuomba kutenguliwa kwa barua ya kujiuzulu kwake.
No comments:
Post a Comment