• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Tuesday, April 4, 2017

    JAPAN YAJIBU VITISHO VYA KOREA KASKAZINI

    Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.
    Katika Mji wa Pyongyang,Kombora lenye uzito wa kati lilirushwa upande wa mashariki mwa bandari ya Sinpo kuelekea bahari ya Japan.
    Waziri kiongozi wa nchi hiyo ,Yoshihide Suga amewaambia waandishi wa habari kuwa nchi yake haiwezi stahimili vitendo hivyo vya uchochezi ambavyo Korea kaskazini imevirudia kuvifanya.
    JapanHaki miliki ya picha
    Image captionMoja ya majaribio ya urushaji wa makombora ya nyuklia unaofanywa na korea kaskazini
    Kombora hilo limerushwa siku chache kabla ya rais wa China, Xi Jinping kufanya ziara nchini Marekani kukutana na rais Trump ili kujadili namna ya kudhibiti mipango ya Nuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini. .

    No comments:

    Post a Comment