• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Wednesday, April 26, 2017

    CHINA YAZINDUA MANOWARI MPYA YA KIVITA




    Haki miliki ya picha

    China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.
    Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.
    Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.
    Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
    Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.

    Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa DalianHaki miliki ya picha
    Image captionMeli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian
    Meli hiyo baada ya kung'oa nanga DalianHaki miliki ya picha
    Image captionMeli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian

    Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.
    China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.

    Liaoning Dalian, 22 Sept 2012Haki miliki ya picha
    Image captionMeli ya kwanza ya kubeba ndege ya China kwa Liaoning ilinunuliwa kutoka Ukraine
    LiaoningHaki miliki ya picha
    Image captionMeli ya Liaoning ilipokuwa inakabidhiwa rasmi kwa jeshi la wanamaji la China Septemba 2012

    No comments:

    Post a Comment