Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kuwa huenda akafuta mipango ya kutafuta pesa za kujenga ukuta wakati wa bajeti wiki hii.
Mshauri wa karibu wa rais Kellyanne Conway, alisema ufadhili wa ukuta huo huenda ukafutwa kwenye bajeti ambayo ni lazima ipitishwe ifikapo Ijumaa.
Ujenzi wa ukuta ambao ungelipigwa na Mexivo ilikuwa ahadi kuu kwenye kampeni ya Trump.
Wanademocrat walikuwa wametisha kuzuia msuada ikiwa pesa zingetengwa kwa ujenzi wa ukuta huo.
Lakini bwana Trump alisisitiza kupitia kwa mtandao wa Twitter kuwa bado alikuwa akiunga mkono ukuta huo na kuwa utajengwa.
Anaripotiwa kuuambia mkutano wa faragha na waandishi wa habari kuwa ataeleza kuhusu kufadhiliwa kwa ukuta huo baadaye mwaka huu.
Wakati Trump aliingia ikulu ya White House alisema kuwa huenda akahitaji pesa za walipa kodi kufadhidli ujenzi wa ukuta, huku pesa zingine zikipatikana kutoka Mexico.
Sasa wakati rais anapokaribia siku zake 100 ofisini, amakumbana na ukuta mwinmgine ambapo maseneta wa Democtrat wanapinga mapendekezo yake.
Trump alikuwa amependekeza dola bilioni 1.5 kwa ukuta wake kama sehemu ya bajeti ya kifadhili mashirika ya serikali.
Wachanganuzi wanasema kuwa rais yuko chini ya shinikizo za kutaka atekeleze ahadi zake za kampeni, ambazo chache zimetekelezwa siku 100 za kwanza akiwa ofisini.
Mkuu wa wafanyakaizi wa rais Reince Priebus, alisema Jumanne kuwa alikuwa akifanya kazi kwa haraka kutekeleza ahadi hizo.
No comments:
Post a Comment