• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Tuesday, May 3, 2016

    TED CRUZ AJITOA KWENYE MCHAKATO WA KUWANIA URAIS WA MAREKANI


    Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro Marekani

    • Saa moja iliyopita
    CruzImage copyrightGetty
    Image captionCruz ameshindwa kwenye mchujo Indiana
    Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.
    Alitoa tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.
    Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika kampeni zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi.
    Mwandishi wa BBC aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.
    TrumpImage copyrightReuters
    Image captionTrump ana nafasi nzuri ya kushinda uteuzi
    Tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.

    No comments:

    Post a Comment