• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, November 5, 2015

    MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO NCHINI TANZANIA.

                                        

                              MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO TANZANIA
                            Dkt John Pombe Magufuli,   Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, katika sherehe zilizofanyka uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
    Mara baada ya kuapa mbele ya Jaji mkuu Mohamed Chande Othman, Dkt Magufuli amepigiwa mizinga 21 kama heshima kwake akiwa pia ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, na kisha kukagua gwaride lenye alama ya alpha  kwa mara ya kwanza akiwa Rais.
    ...
          Baada ya hapo amesalimiana na viongozi wastaafu akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete, Benjamini Mkapa pamoja viongozi mbalimbali kutoka nchi jirani akiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museven wa Uganda.
    Baadaye ndege za kivita zimepita mbele yake kama ishara ya heshima kwa amiri jeshi mkuu.
    Mara baada ya gwaride maalum, zilifuata burudani mbalimbali na kisha Rais Magufuli kutoa neno la shukurani ambapo amewataka watanzania wote kuungana na kuacha tofauti zao za kisiasa ili kufanya kazi kwa maslahi ya taifa.
    Naye Samiah Suluhu Hassan ameapa kuwa makamu wa Rais wa awamu ya tano. Kwa kiapo hicho, Samiah amekuwa ndiye makamu wa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania

    No comments:

    Post a Comment