• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Thursday, November 5, 2015

    DSTV YASHUSHA BEI YA VISIMBUZI VYAKE

                                 KAMPUNI ya MultiChoice Africa inayosambaza visimbuzi vya DStv, imetoa punguzo la manunuzi ya visimbuzi vyake katika msimu huu wa kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka.
    Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Baraka Shelukindo alisema, kuanzia sasa visimbuzi vya DStv vitauzwa Sh 79,000, ikiwa ni pamoja na kupata kifurushi cha mwezi cha DStv Bomba.
    Alisema katika msimu huu wa kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka, kampuni hiyo imeona vema kuwazawadia Watanzania kwa kutoa ofa hiyo pamoja na kuzindua kifurushi cha kitanzania cha DStv Bomba, kinachouzwa Sh 23,500 kwa mwezi.
    Akizungumzia kifurushi hicho ambacho Balozi wake ni mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul (Diamond Platnumz), Shelukindo alisema kina zaidi cha chaneli 65 za vitu tofauti ikiwemo makala, michezo, habari na tamthilia.
    Kwa upande wake, Diamond alisema kifurushi hicho kimekuja kwa wakati kwani watanzania wengi wanapenda kupata chaneli zinazokidhi matakwa yao na kwamba hata bei yake ni nafuu ikilinganishwa na ubora na wingi wa chaneli katika kifurushi hicho. “Ni kifurushi kizuri chenye chaneli zilizo jaa maudhui ya jamii yetu ya Tanzania.


    No comments:

    Post a Comment