• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Monday, May 29, 2023

    WALIMU 30 WANOLEWA MFUMO WA FFARS SERENGETI

     

    Serengeti-Mara

    WALIMU zaidi ya 30 kutoka katika kata 30 za halmashauri ya wilaya ya Serengeti wamepatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya mfumo  wa kielektroniki wa FFARS.Walimu hao kutoka shule za msingi wamepatiwa mafunzo hayo  Ili kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili hapo awali ikiwemo kutumia watu wasio watumishi wa serikali jambo ambalo lilikuwa likihatarisha usalama wa taarifa za serikali 

    Akifungua mafunzo hayo afisa elimu msingi wa halmashauri ya wilaya ya SERENGETI MUJIBU MUSTAPHA BABARA amewataka walimu hao kuwa mabalozi Kwa kueneza elimu hiyo Kwa watumishi ndani ya kata zao.Aidha Bwana Babara amesisitiza umuhimu wa walimu wakuu na wakuu wa shule kuufahamu mfumo huo kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa fedha za serikali katika taasisi zao.Pia Mr Babara ameeleza kuwa atatumia kundi hili la walimu 30 katika kutoa mafunzo ya mfumo ya PReM na S.I.S Ili kuweza kuwajengea uwezo walimu wakuu na walimu wa takwimu  kuwa na ujuzi wa kutosha katika kutumia mifumo hii.

    Akitoa neno Kwa washiriki SLO wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Bwana JAMES JOHANES alisisitiza uzalendo Kwa washiriki kwani Wana nafasi kubwa ya kuisaidia serikali katika kufanikisha mipango yake.

    Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika katika ukumbi wa CRC Mugumu tarehe 27 na 28 Mei 2023.


    Imeandikwa na 

    Frank Obed Lungwa




    No comments:

    Post a Comment