Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya anadaiwa kughushi nyaraka za Idara ya Usalama wa Taifa na kuzitumia kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara mkoani Arusha.
mwenyekiti huyo anadaiwa kutapeli baadhi ya wafanyabiashara kwa kujitambulisha kuwa yeye ni afisa wa usalama wa taifa huku vitendo vyake vikidaiwa kulindwa na viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani Arusha.
Katika tukio moja Sabaya anadaiwa kutumia kitambulisho cha idara ya usalama wa taifa kumtapeli binti mmoja mjini Arusha kiasi cha shilingi milioni 7 kwa ahadi ya kumpatia kazi katika migodi ya Tanzanite iliyopo Mererani Arusha. Licha ya kutapeliwa kiasi hicho cha fedha binti huyo pia aliombwa rushwa ya ngono japo alikataa.
Katika kisa kingine ndugu Sabaya anadaiwa kulala hoteli moja jijini Arusha ijulikanayo kama “Sky Way Hotel” kwa muda wa siku 6 lakini akakataa kulipa. Alipoulizwa alidai yeye ni afisa wa idara ya usalama wa taifa hivyo hawezi kulipa.
Uongozi wa hoteli hiyo ulimzuia kutoka hadi akamilishe kulipa deni hilo lakini Sabaya aliendelea kusisitiza kuwa yeye ni Afisa usalama wa taifa hivyo hatakiwi kulipa. Pia aliutishia kwamba wakiendelea kumsumbua ataifunga au kuwanyang’anya leseni ya kuendesha hoteli hiyo.
Hata hivyo uongozi wa hoteli hiyo haukutishwa na kuamua kumsachi ambapo walikuta hana fedha taslimu lakini walifanikiwa kumnyang’anya vitambulisho vyote na kadi za benki. Kisha wakamfungulia kesi katika kituo cha polisi kati yenye jalada AR\RB5044\2016 ambapo pia waliwasilisha vitambulisho vyake walivyomnyang’anya.
Baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Mwenyekiti huyo alienda kujisalimisha polisi na kulipa deni alilokua anadaiwa na hoteli hiyo kiasi cha shilingi 309,400 na polisi wakamkabidhi vitambulisho vyake. Jambo la ajabu ni kwamba polisi walimrudishia hadi kitambulisho cha kughushi cha usalama wa taifa anachokitumia kutapeli.
Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mtui alisema Mwenyekiti huyo hana makazi rasmi na amekua mtu wa kulala nyumba za wageni, na kufanya starehe kwa pesa anazopewa na vigogo wa CCM na serikali ambao wamekua wakimtumia kuchafua baadhi ya viongozi wa serikali na makada wengine ndani ya CCM”
Uchunguzi uliofanywa imebaini kuwa katika kituo cha polisi kati, Sabaya amewahi kufunguliwa kesi 4 na watu tofauti kwa madai ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lakini hakuna hata kesi moja aliyopelekwa mahakamani.
chanzo.ST tar 15/09/2016

No comments:
Post a Comment