Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba ,kituo cha polisi cha penguria huko nchini Kenya kimevamiwa na mtu aliyejihami kwa silaha.Inasadikika mtu huyo anafanya shambulio hilo ili kumuokoa mwenzake ambaye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za ugaidi.Mtuhumiwa huyo aliyekuwa akishikiliwa na polisi katika kituo hicho naye ameshika silaha na anapambana na polisi.Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation inasadikiwa askari Zaidi ya wane wamekwishapoteza maisha.Polisi Zaidi wametumwa katika eneo hilo ili kukabiliana na wahalifu hao.
No comments:
Post a Comment