• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Wednesday, October 28, 2015

    TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI IMESEMA KUWA MCHAKATO WA UCHAGUZI UTAENDELEA KAMA KAWAIDA TANZANIA BARA

    Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi bwana Damian Lubuva amesema kuwa mchakato wa uchaguzi kwa upande wa Tanzania bara utaendelea kama kawaida kutokana na kwamba tayari walishatangaza matokeo ya uraisi wa jamhuri ya muungano kutoka majimbo yote ya Zanzibar.
           Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutangazia matokeo ya uraisi cha ukumbi wa mwl Nyerere jijini Dar es salaam ,Lubuva amesema hakuna kasoro yoyote iliyojitokeza katika kura za za uraisi visiwani Zanzibar.
           Hayo yanakuja baada ya Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kufuta matokeo ya uchaguzi na uchaguzi kutokana na kasoro kubwa zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo.
           wakati huo huo vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA vimesema havitakubali matokeo yoyote yatakayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kutokana nakuahirishwa kwa uchaguzi huko Zanzibar.

    No comments:

    Post a Comment