Rais mpya wa Marekani Donald Trump amepiga marufuku wakimbizi wote wa Syria kuingia Marekani hadi wakati anasema serikali yake itakuwa imeweka mkakati mkali zaidi wa kuwakagua wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini humo.
Kwa mujibu wa amri hiyo ya Trump, wakimbizi wote wanaofika mipakani mwa Marekani kwa sababu ya kutoroka vita makwao au sababu yoyote nyengine pia hawataruhisiwa kwa sasa kwani maafisa wa uhamiaji wamepewa miezi minne ya kuweka mfumo huo wa upekuzi na ukaguzi wa kina anaouita "extreme vetting". Pia kuna orodha ya mataifa mengine sita ambayo raia wake hawaruhusiwi kupewa visa za Marekani .
Mataifa hayo ni Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen
Bw. Trump anasema mikakati hiyo mipya inalenga kuzuia Waislamu walio na itikadi kali kutoingia kabisa Marekani.
No comments:
Post a Comment