Serikali na makundi ya upinzani nchini DR Congo wanatarajiwa kutia saini makubaliano ya kugawana mamlaka baadaye leo.
Pande hizo mbili zimekaribia kuafikia mwafaka kwa mwezi mmoja sasa.Makubaliano hayo yalioafikiwa na maaskofu wa kanisa katoliki yanaweka ratiba ya kuondoka kwa rais Joseph Kabila ambaye muda wake wa utawala ulikamilika mwezi uliopita.
Pia yanatoa maelezo ya vile serkali hiyo ya mpito itakavyokuwa huku zaidi ya mawaziri 50 na waziri mkuu wakiteuliwa na upinzani.
Uongozi wa rais Kabila wa miaka 16 umezongwa na mapigano kati ya makundi mbalimbali ya waasi mashariki mwa taifa hilo mbali na madai ya ufisadi.
Makumi ya watu wamefariki katika kipindi cha miezi mitatu ambapo waandamanaji wametaka rais Kabila kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment