• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Friday, March 16, 2018

    MAKUMI WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI SERENGETI

    Image may contain: outdoor and nature
    Leo majira ya saa tano za asubuhi,kibayaclassic ilipata taarifa kuhusu ajali iliyolihusisha basi la kampuni ya KIMOTCO GROUP linalofanya safari zake kati ya Arusha na Musoma kupitia katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.Basi hilo limepata ajali katika makao makuu ya hifadhi ya serengeti(seronera)katika mto maarufu ujulikanao kama mto BUNAGI.
       Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema basi hilo lililokuwa likitokea musoma kwenda arusha lilikuwa likijaribu kupita katika mto huo wakati ambapo ulikuwa ukitiririsha maji kwa kasi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi.
       Hata hivyo hakuna vifo vilivyoripotiwa hadi sasa kutokana na ajali hiyo.

    No comments:

    Post a Comment