• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Sunday, March 19, 2017

    HOFU YA UGAIDI WHITE HOUSE


    Kikosi cha kumlinda rais kikipiga doria ikulu
          Mtu mmoja anazuiwa na polisi baada ya kuendesha gari hadi kwenye kuzuizi cha ikulu cha Marekani Jumamosi usiku, kwa mujibu wa kikosi cha kumlinda rais.
    Ulinzi kwenye ikulu ya White House uliongezwa mara moja. Kituo cha CNN kinasema kuwa dereva wa gari hilo alidai kuwa na bomu.
    Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa jimbo la Florida wakati kisa hicho kilitokea.
    Kikosi kinachoilinda ikulu ya White House kinasema kuwa dereva alikaribia kizuizi cha ikulu mwendo wa saa 03:05 GMT
    Kisha dereva wa gari hilo alikamatwa.
    Kisa hicho ndicho cha pili kutokea White House, baada ya mtu mmoja mapema kuruka eneo la kuegeshwa baiskeli kwenye ua unaouzunguka White House.
    Kikosi cha kumlinda rais kimekosolewa vikali wiki hii baada ya kisa cha mtu mmoja kuruka ua tarehe 10 mwezi Machi na kuikaribia ikulu.
    Jonathan Tran mwenye umri 26, alikaa ndani ya uwanja wa White House kwa zaidi ya dakika 16 kabla ya kukamatwa.

    No comments:

    Post a Comment