Rais wa Marekani Barack Obama amelalamika kuhusu huduma ya wi-fi katika ikulu ya White House alipokuwa akihojiwa kwenye runinga.
“Kuna maeneo mengi sana hayana wi-fi,” Rais Obama amefichua akihojiwa kabla ya mchuano wa Super Bowl katika runinga ya CBS.“Huwa inatatiza sana,” ameongeza mkewe Michelle, ambaye amesema mabinti wao Malian a Sasha huudhishwa sana na hilo.
Kwa kawaida, Bw Obama amekuwa akifanya mahojiano ya runinga kabla ya mechi hiyo kuu zaidi katika soka Marekani.
Rais Obama ameongeza kwamba amekuwa akijaribu kuimarisha huduma hiyo “kwa ajili ya jamaa wapya watakaoingia (White House)”.
Bw Obama aliandamana na mkewe kwenye mahojiano hayo kwa mara ya kwanza
No comments:
Post a Comment