• KIBAYACLASSIC

    The voice of Africa

    Saturday, June 17, 2023

    KATA YA NATTA YAKAMILISHA MAFUNZO YA MFUMO WA FFARS

    Tarehe 17 June 2023

    Natta -Serengeti

    Kata ya Natta imefanikiwa kukamilisha mafunzo ya mfumo wa ffars kwa mafanikio makubwa.Mafinzo hayo yaliyoshirikisha walimu wakuu na walimu wa fedha kutoka shule zote zilizopo ndani ya kata ya Natta yamefanyika tarehe 16 June 2023.Akifungua mafunzo hayo mwakilishi wa Afisa elimu kata Bwana Maziba Nashoni aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuchukulia kwa uzito ili kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili hapo awali.

                                     Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja.

    Shule zilizoshiriki mafunzo hayo ni Mlimani shule ya msingi,Kono,Makundusi,Kewambogo,Motukeri,
    Nattabigo,Nyakitono na Makoroboi shule ya msingi.Aidha mafunzo hayo ni ya awali kwani kwa mujibu wa mwezeshaji wa mafunzo hayo bwana Frank Obed Lungwa mafunzo yatakuwa yakifanyika mara kwa mara ili kujenga uwezo zaidi kwa walimu wakuu na walimu wa fedha juu ya matumizi sahihi ya mfumo huo.

    Imeandikwa na Frank Obed Lungwa
    +255783002098


    No comments:

    Post a Comment